Sadio Mane ameumia nyama za paja akiichezea Senegal Jumamsi na atakuwa nje kwa wiki sita PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KLABU ya Liverpool imepata pigo kufuatia habari kwamba mshambuliaji Sadio Mane ameumia nyama za paja na anatakiwa kuwa nje kwa wiki sita.
Mane, ambaye amefunga mabao matatu kwenye mechi nne za Ligi Kuu ya England hadi sasa msimu huu, alitolewa dakika ya 89 Jumamosi Senegal ikishinda 2-0 dhidi ya Cape Verde kwenye mechi ya kufuzu Kombe Ia Dunia.
Mchezo wa kwanza atakaoukosa ni wa nyumbani dhidi ya Manchester United Jumamosi. Wiki sita ambazo atakaa nje, atakosa mechi nane za Liverpool, ukiwemo wa Ligi Kuu wa nyumbani dhidi ya Chelsea.
Mane ni tegemo katika mfumo wa kocha Mjerumani, Jurgen Klopp Liverpool na kukosekana kwake ni pigo.
Liverpool inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 12 kutoka mechi zao saba za mwanzoni na wametoa sare mechi zao mbili za mwanzo za Ligi ya Mabingwa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, Mane tayari amekosa mechi tatu msimu huu alipokuwa akitumikia adhabu baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea rafu kipa wa Manchester City, Ederson mwezi uliopita katika mchezo wa Ligi Kuu.
Klopp sasa atalazimika kuchagua wachezaji wengine wa kutumia kipindi hiki hadi Mane atakaporejea mwishoni mwa Novemba.
Washambuliaji Daniel Sturridge na Dominic Solanke watagombea nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza, wakati Philippe Coutinho, Roberto Firmino na Mohamed Salah wanaweza kuanzishwa pamoja pia kwenye safu ya ushambuliaji.
0 comments:
Post a Comment