// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LIPULI ‘YAWALIPUA’ 3-0 LEICESTER CITY MECHI YA KIRAFIKI KILWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LIPULI ‘YAWALIPUA’ 3-0 LEICESTER CITY MECHI YA KIRAFIKI KILWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, October 03, 2017

    LIPULI ‘YAWALIPUA’ 3-0 LEICESTER CITY MECHI YA KIRAFIKI KILWA

    Na Gharib Mzinga, KILWA
    TIMU ya Lipuli FC ya Iringa jana imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Leicester City katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Ukote Mjini, Kilwa Kivinje,.
    Mabao ya Lipuli yote yalipatikana kipindi cha kwanza katika mchezo huo yakifungwa na Freddy Tangalu dakika ya 21, Chona Mwangonela dakika ya 33 na Jerome Lembele dakika ya 40.
    Na kipindi cha pili kilikua kigumu kutokana na wachezaji wa Leicester City kuwazoea wapinzani wao na kuanza kupambana nao bila woga, ingawa sifa zadi zimuendee kipa namba mbili aliyeingia kipindi cha pili, Mfaume Mussa aliyewazuia wageni kuongeza mabao.
    Wachezaji wa Lipuli FC kabla ya mchezo wa jana dhidi wenyeji, Leicester City
    Wachezaji wa Leicester City kabla ya mchezo dhidi ya Lipuli FC jana

    Nyota wa mchezo huo alikuwa ni mshambuliaji wa zamani wa Azam FC na Ruvu Shooting, Seif Abdallah Karihe wa Lipuli aliyeisumbua mno ngome ya Leicester City,. 
    Mgeni rasmi alikua mheshmiwa mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini, Suleiman Bungara ‘Bwege’ na Lipuli iliingia kwenye mchezo huo ikitoka Mtwara, ambako Jumamosi ilifungwa 2-1 na wenyeji, Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Moja kwa moja, Lipuli ya kocha Suleiman Matola inarejea Iringa kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu dhidi ya jirani zao, Njombe Mji FC Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe, Oktoba 14, mwaka huu.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIPULI ‘YAWALIPUA’ 3-0 LEICESTER CITY MECHI YA KIRAFIKI KILWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top