KLABU ya Bayern Munich inajiandaa kumrejesha Jupp Heynckes kutoka kwenye kustaafu afundishe kwa mara ya nne khistoria klabu hiyo ya Bavaria.
Kwa mujibu wa taarifa nchini Ujerumani, Bayern imekubali Heynckes mwenye umri wa miaka 72 achukue nafasi ya Carlo Ancelotti aliyefukuzwa wiki iliyopita.
Katika msimu wake wa mwisho na vigogo hao wa Bundesliga mwaka 2013, Heynckes aliiongoza timu hiyo kubeba mataji matatu, kisha akastaafu na nafasi yake kuchukuliwa na Pep Guardiola.
Jupp Heynckes anatarajiwa kurejea Bayern Munich kama kocha kwa mara ya nne kihistoria PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Gazeti la Bild la Ujerumani limeandika: 'Mataji matatu anasemekana kuwa sahihi, radhi, kihistori na kwa kazi nzuri aliyowahi kufanya. Na vipi anarejea,".'
Mkongwe huyo inasemakana anarejeshwa kama suluhisho la muda mfupi kwa mabingwa hao wa Ujerumani.
Heynckes anaifahamu klabu na ligi baada ya kufundisha kwa mudamrefu awali.
Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1987 hadi 1991 kipindi ambacho aliiongoza timu kutwaa mataji mawili.
Akarejeshwa tena kama kocha wa muda mwaka 2009 akichukua nafasi ya Jurgen Klinsmann aliyefukuzwa zikiwa zimebaki mechi tano ili kumalizika kwa msimu.
Akaiwezesha timu kutoa sare moja na kushinda mechi nne, hivyo kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Bundesliga na kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Akaenda kufundisha Bayer Leverkusen kwa miaka miwili kabla ya kurejea Bayern kuchukua nafasi ya Louis van Gaal msimu wa 2011-2012.
Msimu wa kwanza Heynckes alishika nafasi ya pili kwenye michuano mitatu, kabla ya msimu uliofuata kupata mafanikio ya kukumbukwa.
Guardiola alitangazwa anakwenda kuwa kocha mpya wa Bayern Munich wakati Heynckes akiwa ameipa timu mataji ya Bundesliga, Kombe la Ujerumani na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Heynckes hakutaka kabisa kurudi kufundisha tena; "Naweza kukuhakikishia kwamba sina dhamira ya kufundisha tena. Nimekuwa na mwisho wa thamani,".
Lakini inaonekana kama mzee huyo wa miaka 72, mshambuliaji wa zamani wa Borussia Mongchengladbach anaweza kurejea kwa mara nyingine.
Anajiandaa kuichukua Bayern ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, ikizidiwa pointi tano na vinara Borussia Dortmund.
0 comments:
Post a Comment