Ratiba kamili ya mechi za mchujo za kufuzu Kombe la Dunia ambazo zitachezwa Novemba 9 hadi 14 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
TIMU ya taifa ya Italia itamenyana na Sweden katika mchezo wa mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi.
Katika droo maalum iliyopangwa mjini Zurich, Uswisi yalipo makao makuu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Ireland ya Kaskazini itamenyana na Uswisi.
Kikosi cha Martin O'Neill kilihofia sana kupangwa na Itali na imekuwa bahati yao wameangukia Uswisi.
Jamhuri ya Ireland yenyewe itamenyana na Denmark, wakati Croatia itamenyana na Ugiriki.
Mechi za kwanza zinatarajiwa kuchezwa kati ya Novemba 9 na 11 na za marudiano Novemba 12-14, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment