Mwonekano wa jengo la makao makuu ya klabu ya Yanga, upande wa Uwanja wa Kaunda liliopo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam ulivyoathiriwa na kufurika kwa madimbwi ya maji katika eneo la Jangwani
Angalau mwonekano wa jengo unakuwa wa kuvutia kidogo unapopanda juu, ingawa kupauka kwa rangi na kuchakaa kwa jengo lenyewe ni tatizo lingine
Mandhari ya jengo la klabu hiyo inapoteza mvuto wake kila kukicha tangu likarabatiwe kwa mara ya mwisho 2008
Mbele ya jengo kuna kifusi kinalundikwa kwa ajili ya kuukarabati Uwanja wa Kaunda uanze kutumika tena
Uongozi umesema umedhamiria kuurudisha Uwanja wa Kaunda katika ubora wake
Pembezoni mwa ukuta wa uzio wa Uwanja wa Kaunda kuna mfereji wa maji, ambao kama yanakuwa yanakwenda vizuri kwenye mkondo wake hayawezi kuingia ndani
Hapa ni katikati ya Uwanja wa Kaunda, ambao kihistoria umeibua vipaji vya wanasoa wengi nyota enzi zake
Tangu 2013 Uwanja wa Kaunda umetelekezewa kabisa na matokeo yake ndiyo haya
Hata jengo nalo linazidi kuchakaa kila kukicha, wakati ni mwaka 2013 tu lilikuwa katika mwonekano mzuri
Jengo la Yanga lipo barabarani kabisa makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani
Jengo la Yanga lipo barabarani kabisa makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani
0 comments:
Post a Comment