// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); GULAM WA TOC AWA MWENYEITI MPYA WA BARAZA LA MICHEZO ZANZIBAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE GULAM WA TOC AWA MWENYEITI MPYA WA BARAZA LA MICHEZO ZANZIBAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, October 18, 2017

    GULAM WA TOC AWA MWENYEITI MPYA WA BARAZA LA MICHEZO ZANZIBAR

    Na Salum Vuai, ZANZIBAR
    BARAZA la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ), limepata Mwenyekiti mpya.
    Katika uteuzi wa viongozi kwenye taasisi mbalimbali za serikali uliofanywa jana Oktoba 17, 2017 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Gulam Abdulla Rashid ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa baraza hilo.
    Dk. Shein amemfanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 7(2) cha sheria ya Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar namba 5 ya mwaka 2010. 

    Rais wa TOC Gulam Abdalla Rashid (kulia), sasa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar  

    Rashid ambaye pia ni Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), anapokea kijiti hicho kutoka kwa Sharifa Khamis Salim ‘Sherry’ aliyekuwa akiishikilia nafasi hiyo kwa miaka mingi.
    Mwenyekiti huyo mpya pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa iliyokuwa Idara ya Michezo Zanzibar ambayo imefutwa miaka mingi sasa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GULAM WA TOC AWA MWENYEITI MPYA WA BARAZA LA MICHEZO ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top