KOCHA Ronald Koeman amefukuzwa na klabu ya Everton baada ya miezi 16 kazini kufuatia matokeo mabaya mwanzoni mwa msimu, ambayo yameifanya timu hiyo ishike nafasi ya tatu kutoka mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England.
Mholanzi huyo ametaarifiwa leo na Mwenyekiti, Bill Kenwright na mwanahisa mkuu wa klabu, Farhad Moshiri kwamba huduma zake zimesitishwa baada ya Everton kufungwa na Arsenal jana.
Alianza kulalamikiwa baada ya matokeo mabaya licha ya kutumia Pauni Milioni 140 wakati wa usajili pamoja na Mkurugenzi wa Soka, Steve Walsh.
Na inaonekana kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 23, David Unsworth ataishika timu kwa sasa kuelekea mchezo wa Jumatano wa Kombe la Carabao dhidi ya Chelsea na wa Ligi Kuu Jumapili dhidi ya Leicester City.
Unsworth, aliisimamia timu katika mchezo wa mwisho msimu wa 2015-2016 wakati Roberto Martinez alipofukuzwa.
Everton itatulia kwanza kabla ya kumteua kocha wa kudumu na tayari kuna makocha kadhaa wanawania nafasi hiyo, wakiongozwa na kocha wa Burnley, Sean Dyche na kocha wa Watford, Marco Silva.
Thomas Tuchel, ambaye hana kazi baada ya kuondoka Borussia Dortmund, na Carlo Ancelotti pia anaweza kuvutiwa na nafasi hiyo ya kazi katika Ligi Kuu.
Koeman anaweza kunufaika na malipo ya baada ya kusitishwa kwa mkataba wake, ambao alikuwa analipwa Pauni Milioni 6 kwa msimu - na kaka yake Erwin, pamoja na kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili, Jan Kluitenburg pia wanatarajiwa kuondoka.
Taarifa iliyotolewa Jumatatu mchana imesema; "Klabu ya soka ya Everton inathibitisha kwamba Ronald Koeman ameondoka klabuni.
"Mwenyekiti Bill Kenwright, Bodi ya Wakurugenzi na mwanahisa mkuu, Farhad Moshiri kwa pamoja wangependa kumshukuru Ronald kwa huduma zake alizotoa katika klabu kwa zaidi ya miezi 16 iliyopita na kuiwezesha klabu kumaliza nafasi ya saba msimu uliopita wa Ligi Kuu,".
Saa kadhaa kabla ya kufukuzwa kwake, Koeman alionekana kwenye mgahawa wa Kitaliano, San Carlo katikati ya Manchester akipata chakula cha usiku San Carlo in central Manchester.
Alikuwea akifurahia chakula hicho na mkewe, Bartina, na kikundi cha marafiki kabla hawajakwenda kwenye klanbu ya usiku kwa starehe zaidi. Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola pia alipata chakula San Carlo katika usiku huo huo.
0 comments:
Post a Comment