Bayern Munich imetangaza kumrejesha kocha wake wa zamani, Jupp Heynckes kuchukua nafasi ya Carlo Ancelotti PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KLABU ya Bayern Munich imetangaza kumrejesha kocha wake wa zamani, Jupp Heynckes, ambaye ataiongoza timu kwa muda hadi mwishoni mwa msimu kufuatia kuondoka kwa Carlo Ancelotti.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 72 hajafundisha klabu tangu alipoondoka Bayern Munich akiiachia mataji matatu msimu wa 2012-13, lakini analazimika kurejea kazini akitoka kustaafu.
Heynckes amesema: "Nisingerudi kwenye klabu nyingine yoyote duniani, lakini Bayern Munich ni kazi ya mapenzi kwangu. Makocha wangu wasaidizi na mimi sasa nitafanya kila kitu kurejesha mafanikio kwa mashabiki wa soka. Ninaangali mbele sana juu ya changamoto hii,".'
Mtendaji Mkuu, Karl-Heinz Rummenigge amesema: "Kuna imani kubwa baina ya Jupp Heynckes na Bayern. Tunamshukuru sana Jupp kwamba amekubakli ofa ya kuwa kocha mkuu. Ni mtu bora kwa wakati huu Bayern,".'
0 comments:
Post a Comment