// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC WASEMA MECHI NA MBEYA CITY ILIKUWA SHUGHULI NZITO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC WASEMA MECHI NA MBEYA CITY ILIKUWA SHUGHULI NZITO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, October 29, 2017

    AZAM FC WASEMA MECHI NA MBEYA CITY ILIKUWA SHUGHULI NZITO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    LICHA ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City usiku wa juzi, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche, amedai kuwa haikuwa mechi nyepesi kutokana na upinzani mkubwa ulioonyeshwa na wapinzani wao.
    Bao pekee lililoipa Azam FC pointi tatu, lilifungwa na Mchezaji Bora wa Azam FC (NMB Player of the Month) mwezi Septemba-Oktoba, mshambuliaji Mbaraka Yusuph, akitumia vema kona iliyochongwa na winga Enock Atta na mpira kumgonga mgongoni baada ya kumponyoka kipa wa Mbeya City, Owen Chaima.
    Mbaraka Yusuph juzi aliifungia bao pekee Azam FC ikishinda 1-0 dhidi ya Mbeya City 

    Cheche amesema kuwa mechi hiyo ilikuwa na ushindani mkubwa kuanzia mwanzo hadi mwisho huku akidokeza kwamba kama mechi zote za ligi zingekuwa zikichezwa kwa kiwango hicho basi soka la Tanzania lingepiga hatua.
    “Nafurahi kwa ushindi na vile vile nafurahi kwa kiwango na ushindani tuliokutana nao katika mechi, kama tunakuwa tunacheza ligi katika mechi zote kwa namna hii nafikiri kiwango chetu cha mpira Tanzania kingekwenda juu, lakini inatokezea baadhi ya mechi moja moja mechi nyingi zinakuwa na matatizo,” alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC WASEMA MECHI NA MBEYA CITY ILIKUWA SHUGHULI NZITO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top