// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA KOMBAINI YA MABATINI KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA KOMBAINI YA MABATINI KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, October 17, 2017

    AZAM FC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA KOMBAINI YA MABATINI KESHO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Azam FC, inatarajiwa kukipiga dhidi ya Mabatini Kombaini katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Alliance kesho Jumatano kuanzia Saa 10.00 jioni.
    Kikosi cha Azam FC kipo hapa mkoani Mwanza tokea juzi, kikifanya maandalizi ya kuikabili Mbao, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) unaotarajiwa kufanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
    Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii na Kombe la Mapinduzi msimu uliopita wanaodhaminiwa na Maji Safi ya Uhai Drinking Water, Benki Bora ya NMB na Tradegents, wanatarajia kuutumia mchezo huo wa kirafiki kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wao na Mbao.
    Hadi hivi wachezaji wote wa Azam FC wako fiti, isipokuwa kipa Razak Abalora, anayesumbuliwa na Malaria, ambaye leo ameanza mazoezi mapesi wakati kikosi hicho kilipofanya mazoezi ya asubuhi katika Uwanja wa Nyamagana, jijini hapa Mwanza.
    Kueleka mchezo wa Mbao, Azam FC imeonekana kuwa kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa ni miongoni mwa timu nne zilizokaa kileleni zote zikiwa na pointi 12, zingine zilizojuu yake zikiwa ni Simba, Yanga na Mtibwa Sugar, ambazo ziko juu yake kwa idadi ya mabao ya kufunga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA KOMBAINI YA MABATINI KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top