TIMU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imejiweka katika nafasi nzuri ya kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa ugenini wa mabao 2-1 jana dhidi ya Al Hilal Al Ubayyid Uwanja wa Al Abyed, Khartoum, Sudan.
Katika mchezo huo, wenyeji walitangulia kwa bao la Kevin Zatu aliyejifunga dakika ya 23, kabla ya Ben Malango Ngita kuwazawazishia mabingwa hao wa zamani wa Afrika dakika ya 30 na kufunga la pili dakika ya 83 kwa penalti.
Mazembe sasa watakuwa na kazi rahisi kwenye mchezo wa marudiano Septemba 24 mjini Lubumbashi, wakihitaji hata sare ili kuingia Nusu Fainali.
Mechi nyingine za Robo Fainali ya michuano hiyo jana, MC Alger ilishonda 1-0 nyumbani dhidi ya Club Africain ya Tunisia, bao pekee la Hichem Nekkache dakika ya tisa Uwanja wa Julai 5, wakati FUS Rabat ilishinda 1- 0 dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia, bao pekee la Karim Benarif kwa penalti dakika ya 19 Uwanja wa Moulay Hassan.
Awali ya hapo, Robo fainali ya kwanza baina ya wenyeji SuperSport United na ZESCO United ya Zambia ilimalizika kwa sare ya 0-0 Uwanja wa Lucas Moripe mjini Pretoria
0 comments:
Post a Comment