Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha Ruvu Shooting kinatarajia kuondoka nchini kesho kwenda mkoani Iringa kwa ajili ya mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Lipuli FC Jumamosi kwenye Uwanja wa Samora uliopo mkoani Iringa.
Ruvu Shooting waliuanza vibaya msimu wa Ligi Kuu baada ya kufungwa mabao 7-0 na Simba SC Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam Agosti 26, mwaka huu kabla ya kwenda kulazimisha sare ya 1-1 na Kagera Sugar mjini Bukoba mwishoni mwa wiki.
Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba wachezji wote wana hali nzuri na leo wanaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wao wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani kabla ya safari yao kesho.
“Tunamshukuru Mungu tunaendelea vizuri japokuwa matokeo yanatuumiza, tunakiri kuwa tumeanza Ligi vibaya na timu inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wetu uliopo Mabatini na naimani tutafanya vizuri dhidi ya Lipuli siku ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Samora mkoani Iringa na tunatarajia kuondoka kesho asubuhi kuelekea mkoani humo kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Lipuli,”amesema Bwire

0 comments:
Post a Comment