// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RAYON KUFUNGUA DIMBA NA AS KIGALI LIGI KUU YA AZAM RWANDA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RAYON KUFUNGUA DIMBA NA AS KIGALI LIGI KUU YA AZAM RWANDA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, September 08, 2017

    RAYON KUFUNGUA DIMBA NA AS KIGALI LIGI KUU YA AZAM RWANDA

    Na Canisius Kagabo, KIGALI
    MABINGWA wa Ligi Kuu ya Azam Rwanda, Rayon Sports wataanza kutetea taji lao katika msimu mpya kwa kumenyana na AS Kigali Septemba 29, Uwanja wa Kigali, Nyamirambo.
    Hiyo ni katika Ratiba ya Ligi Kuu ya Azam Rwanda maarufu kama ‘Azam Rwanda Premier League’, msimu wa 2017/2018 iliyotolewa jana Shirikisho la Soka nchini Rwanda (FERWAFA).
    Kikao cha Kamati ya Utendaji ya FERWAFA kilichofanyika jana kiliamua kwamba ligi inapaswa kuanza mwishoni mwa mwezi wa Septemba na kuwakumbusha viongozi wa klabu kutafuta vitambulisho (license) vya wachezaji wake mapema.
    “Nataka kuwaambia kwamba leo kamati ya Utendaji ya FERWAFA tumefanya kikao kirefu, tumethibitisha kwamba ligi itaanza tarehe 29 mwezi Septemba mwaka 2017. Tunawakumbusha viongozi wa klabu kutafuta vitambulisho vya wachezaji wao mapema,” amesema Makamu wa Rais wa FERWAFA, Kayiranga Vedaste. 
    Si kawaida kwa Ligi Kuu ya Azam Rwanda kuanza mapema, lakini msimu huu FERWAFA imeonyesha mabadiliko mapema, kuashiria msimu mpya utakuwa mzuri.

    RATIBA YA MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU YA AZAM RWANDA
    Septemba 29, 2017
    Rayon Sports vs AS Kigali
    Septemba 30, 2017
    APR FC vs Sunrise FC
    Etincelles FC vs Police FC
    Gicumbi FC vs Espoir FC
    Kirehe FC vs Mukura VS
    Oktoba 1, 2017
    Bugesera FC vs Amagaju FC
    Miroplast FC vs Marines FC
    Kiyovu Sports vs Musanze FC
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAYON KUFUNGUA DIMBA NA AS KIGALI LIGI KUU YA AZAM RWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top