Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA wa Simba, Joseph Marius Omog anaendelea vizuri baada ya kugongana na mchezaji wake, Mganda Emmanuel Okwi jana mazoezini Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Taarifa ya Simba SC leo imesema kwamba kocha huyo Mcameroon leo ameendelea kukiandaa kikosi chake kwa ajili ya mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mwadui.
Simba watakuwa wenyeji wa Mwadui FC ya Shinyanga Jumapili Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuu – na leo Omog akisaidiana na Mganda, Mayanja ameendelea kukinoa kikosi hicho kuelekea mchezo huo wa tatu wa Ligi Kuu, baada ya kuvuna pointi nne katika mechi mbili za awali.
Kocha Joseph Omog anaendelea vizuri baada ya kugongana na mchezaji wake, Mganda Emmanuel Okwi jana mazoezini Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam
Simba iliuanza msimu mpya wa Ligi Kuu kwa kishindo, ikiifumua Ruvu Shooting mabao 7-0 Agosti 26, kabla ya kwenda kulazimisha sare ya 0-0 na Azam FC Septemba 9, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Kwa ujumla, Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki na Ijumaa Azam FC watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar Uwanja wa Azam Complex, wakati Jumamosi, mabingwa watetezi, Yanga watakuwa wageni wa Maji Maji Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
Mechi nyingine za Jumamosi, Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Mbao FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, Tanzania Prisons wataikaribisha Ndanda FC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Lipuli FC watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Samora mjini Iringa na Stand United wataikaribisha Singida United Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mchezo mwingine wa Jumapili mbali na Simba na Mwadui ni kati ya wenyeji, Mbeya City dhidi ya Njombe Mji FC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

0 comments:
Post a Comment