// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MSUVA ALAZIMISHWA SARE MOROCCO, AUKATAA ‘UCHEZAJI BORA HEWA’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MSUVA ALAZIMISHWA SARE MOROCCO, AUKATAA ‘UCHEZAJI BORA HEWA’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, September 14, 2017

    MSUVA ALAZIMISHWA SARE MOROCCO, AUKATAA ‘UCHEZAJI BORA HEWA’

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana amecheza kwa dakika zote 90 timu yake, Difaa Hassan El - Jadida ikilazimishwa sare ya 0-0 na Ittihad Tanger katika mchezo wa Kombe la FA Morocco Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan.
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online usiku wa jana baada ya mechi, Msuva alisema kwamba walikuwa wana mechi ngumu jana kwa sababu walikutana na wapinzani wazuri.
    Simon Msuva (kulia) akiwa na mpira pembeni ya mchezaji wa Ittihad Tanger 
    Wchezaji wa Ittihad Tanger wakipapatika na mpira mbele ya Simon Msuva
    Simon Msuva katika kikosi cha kwanza cha Difaa Hassan El-Jadida jana 

    “Ilikuwa mechi ngumu sana, jamaa wazuri sana, lakini tutajitahidi tushinde mechi ya marudiano kwao tusonge mbele,”alisema Msuva.
    Mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola kati ya Difaa Hassan El – Jadida na FUS Rabat uliokuwa ufanyike leo Uwanja wa FUS, Hay Nahda mjini Rabat umeahirishwa.
    Difaa sasa watasafiri kuifuata Ittihad Tanger Septemba 20 kwa mchezo wa marudiano wa Kombe la FA.
    Wakati huo huo: Simon Msuva amekanusha uvumi kwamba yeye ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa klabu yake, Difaa Hassan El- Jadida.
    “Kaka hizi habari mimi sijui hata zinatoka wapi, hakuna kitu kama hicho. Ni habari za uongo,”amesema Msuva.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSUVA ALAZIMISHWA SARE MOROCCO, AUKATAA ‘UCHEZAJI BORA HEWA’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top