Na Mwandishi Wetu, MBEYA
KLABU ya Mbeya City FC leo imesitisha mkataba na aliyekuwa kocha wake Mkuu, Mmalawi Kinnah Phiri.
Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha kilichofanyika leo mjini Mbeya, kufuatia malalamiko ya kocha huyo kutolipwa mishaharakwa miezi mitano kiasi cha kususa.
Kikao cha leo kilikuwa ni mwendelezo wa vikao kadhaa baina ya pande hizo mbili tangu Julai mwaka huu na baada ya majadiliano marefu, Mbeya City na Phiri wamekubaliana kutoendelea kufanya kazi pamoja.
"Sababu kubwa ni matokeo mabaya ya timu ya msimu uliopita 2016/2017 ambayo yameipunguzia klabu uwezo mkubwa wa kuhimili mahitaji yake ya msingi baada ya wadhamini waliotarajia kuingia kushindikana na wadhamini waliopo kupunguza kiwango cha udhamini wao kutokana na matokeo hayo yasiyoridhisha,"imesema taarifa ya Mbeya City.
Kocha Mmalawi, Kinnah Phiri leo ametupiwa virago rasmi Mbeya City
Wakati uongozi ukiendelea kutafuta kocha mpya, kwa sasa Mbeya Citu ipo chinio ya mchezaji wake wa zamani na aliyekuwa Kocha Msaidizi tangu wakati wa Juma Mwambusi, Mohammed Kijuso."Klabu inapenda kumshukuru Kocha Phiri kwa mchango wake muhimu katika timu yetu, itaendelea kuuthamini na kuukumbuka na inaamini Kocha Phiri ataendelea kuwa msaada katika maendeleo ya timu yetu kwani amekuwa sehemu ya familia yetu,"imesema taarifa ya MCC.

0 comments:
Post a Comment