Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
UONGOZI wa klabu ya Maji Maji FC ya Songea umesema kwamba umesema unalazimika kubuni vyanzo vingine vya kimapato ili kuweza kujimudu, kwani udhamini wa kampuni ya SokaBet pekee hautoshelezi.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Maji Maji iliyopo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu wa tatu mfululizo tangu ipande tena, Onesmo Ndunguru leo katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari.
“Uongozi wa Klabu ya Maji Maji yenye makao makuu Songea Ruvuma Tanzania siku ya tarehe 19 /09/2017 ilitoa namba maalumu kwa ajili ya wadau mbalimbali wakereketwa, wanachama na wapenzi wa Klabu hiyo popote walipo Tanzania kuweza kuichangia kwa kiwango chochote ambacho watajaliwa nacho ili kuiwezesha kujiendesha katika Ligi Kuu,”amesema Ndunguru.
Afisa Habari huyo amesema kwamba pamoja na mengine yote, klabu pia imeona ni bora ibuni njia mbalimbali za kuweza kujipatia kipato ili iweze kuepukana na hali ngumu ya kiuchumi inayoikabili kwa sasa.
“Klabu ina vyanzo kadhaa vya Mapato ikiwemo jezi za Mashabaiki ambazo zipo mtaani hivi sasa na bado uongozi unaendelea kutafuta Vyanzo mbalimbali vya mapato na wadhamini mbalimbali pia ili Klabu iishi vizuri,”.
“Tunashukuru sana Uongozi wa Sokabet kwa kukubali kutudhamini kwa mkataba wa mwaka mmoja, sasa hapa kuna baadhi ya wadau mbalimbali kama panawachanganya kidogo, SokaBet wao wamechukua upande wa mishahara kwa wachezaji na benchi la ufundi kwa mwaka huo mmoja. Sasa kama bodi bado ina kazi ya kufanya, maanake kuna uendeshaji mwingine katika klabu kama vile kambi, chakula, safari na kadhalika,”amesema.
UONGOZI wa klabu ya Maji Maji FC ya Songea umesema kwamba umesema unalazimika kubuni vyanzo vingine vya kimapato ili kuweza kujimudu, kwani udhamini wa kampuni ya SokaBet pekee hautoshelezi.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Maji Maji iliyopo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu wa tatu mfululizo tangu ipande tena, Onesmo Ndunguru leo katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari.
“Uongozi wa Klabu ya Maji Maji yenye makao makuu Songea Ruvuma Tanzania siku ya tarehe 19 /09/2017 ilitoa namba maalumu kwa ajili ya wadau mbalimbali wakereketwa, wanachama na wapenzi wa Klabu hiyo popote walipo Tanzania kuweza kuichangia kwa kiwango chochote ambacho watajaliwa nacho ili kuiwezesha kujiendesha katika Ligi Kuu,”amesema Ndunguru.
Baadhi ya wachezaji wa Maji Maji kutoka kulia Abdulhalim Humud, Kennedy Kipepe na Jerson Tegete |
“Klabu ina vyanzo kadhaa vya Mapato ikiwemo jezi za Mashabaiki ambazo zipo mtaani hivi sasa na bado uongozi unaendelea kutafuta Vyanzo mbalimbali vya mapato na wadhamini mbalimbali pia ili Klabu iishi vizuri,”.
“Tunashukuru sana Uongozi wa Sokabet kwa kukubali kutudhamini kwa mkataba wa mwaka mmoja, sasa hapa kuna baadhi ya wadau mbalimbali kama panawachanganya kidogo, SokaBet wao wamechukua upande wa mishahara kwa wachezaji na benchi la ufundi kwa mwaka huo mmoja. Sasa kama bodi bado ina kazi ya kufanya, maanake kuna uendeshaji mwingine katika klabu kama vile kambi, chakula, safari na kadhalika,”amesema.
0 comments:
Post a Comment