// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LWANDAMINA AFURAHIA KUREJEA KWA AMISSI TAMBWE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LWANDAMINA AFURAHIA KUREJEA KWA AMISSI TAMBWE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, September 26, 2017

    LWANDAMINA AFURAHIA KUREJEA KWA AMISSI TAMBWE

    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa Yanga SC, Mzambia, George Lwandamina ameweka matumaini makubwa kwa mshambuliaji wake Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe aliyeanza mazoezi jana baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na maumivu ya goti.
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo asubuhi, Lwandamina amesema kwamba amefarijika na kurejea kwa Tambwe ambaye alianza rasmi mazoezi jana, kwani mchezaji huyo ni mjuzi na mzoefu.
    Lwandamina amesema kwamba Tambwe ni mshambuliaji anayejua majukumu yake vizuri na ambaye kukosekana kwake kumeipunguzia makali safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.
    Amissi Tambwe akiwa mazoezini na Yanga leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam

    Kukosekana kwa Amissi Tambwe wazi kumepunguza makali ya safu ya ushambuliaji ya Yanga 
    “⁠⁠Ameanza mazoezi jana, hivyo bado ni mapema kusema chochote juu ya namna alivyoimarika, anahitaji muda kidogo,”amesema Lwandamina.
    Tambwe aliumia mapema Agosti katika kambi ya mazoezi kisiwani Pemba kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wa jadi, Simba SC uliofanyika Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na Yanga kufungwa kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
    Lakini maumivu hayo yalikuwa ni kama kutonesha maumivu yake ya msimu uliopita yaliyomuweka nje kwa muda mrefu pia.
    Yanga ipo katika maandalizi ya mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
    Mabingwa hao watetezi, tayari wamekwishacheza mechi nne hadi sasa, wakishinda mbili na kutoa sare mbili, ingawa makali ya safu ya ushambuliaji yamepungua kutokana na kuvuna bao moja katika kila mchezo, sare za 1-1 na Lipuli na Maji Maji na ushindi wa 1-0 dhdi ya Njombe Mji na Ndanda FC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LWANDAMINA AFURAHIA KUREJEA KWA AMISSI TAMBWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top