Na Mwandishi Wetu, MBEYA
KLABU ya Maji Maji ya Songea mkoani Ruvuma imepata pigo kufuatia kukimbiwa na kocha wake, Kali Ongala baada ya kushindwa kumlipa mishahara kwa miezi miwili, kiasi cha Sh. Milioni 27.
Hayo yamejulikana leo wakati Maji Maji ikiwa mjini Mbeya tayari kwa mchezo wake wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara keshokutwa dhidi ya wenyeji Tanzania Prisons, Uwanja wa Sokoine mjini Mbeyaa bila kocha wake huyo.
Msemaji wa Maji Maji, Onesmo Emillian ameithibitishia Bin Zubeiry Sports – Online leo mjini Mbeya kwamba juu ya kuondoka kwa Ongala, aliyeisaidia timu hiyo kuepuka kushuka Daraja kwa misimu miwili mfululizo iliyopira.
Kali Ongala ameondoka Maji Maji baada ya kushindwa kumlipa mishahara kwa miezi miwili Sh. Milioni 27
“Kali ameandika barua ya kujiuzulu akisema anaondoka kwa sababu klabu imeshindwa kumlipa mishahara yake kwa miezi miwili, kwa hivyo kwa sasa hatupo naye,”alisema.
Hata hivyo, Msemaji huyo alisema kwamba uongozi wa Maji Maji siyo unaopaswa kumlipa fedha hizo Kali, bali ni wafadhili wa timu hiyo, kampuni ya GSM ndiyo iliyoingia naye mkataba.
Maji Maji imeuanza msimu mpya kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mbeya City katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu iliyopita Uwanja wa Sokopine mjini Mbeya na keshokutwa itarudi kwenye Uwanja huo kwa mchezo mwingine dhidi ya Prisons.

0 comments:
Post a Comment