Frank De Boer amefukuzwa Crystal Palace baada ya matokeo mabaya Ligi Kuu ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KOCHA Frank de Boer amefukuzwa katika klabu ya Crystal Palace leo na nafasi yake itachukuliwa na Roy Hodgson Uwanja wa Selhurst Park.
De Boer anafukuzwa kutokana na matokeo mabaya, baada ya kushindwa kupata japo pointi au kufunga bao moja katika mechi nne za awali za Ligi Kuu ya England, ikiwemo ya Jumapili ambayo walifungwa na Burnley.
Hodgson anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili The Eagles baada ya kumzidi kocha mwenzake wa zamani wa England, Hodgson na Sam Allardyce waliyekuwa naye sambamba katika kwenye mbio za kuwania nafasi hiyo.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka The 70 anatarajiwa kurejea kwenye Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza tangu alipoondoka West Brom kujiunga na timu ya taifa mwaka 2012, baada ya awali kuzifundisha Liverpool, Fulham na Blackburn katika michuano hiyo mikubwa ya klabu nchini humo.
Amekuwa nje ya kazi tangu England ivurunde kwenye michuano ya Euro 2016, ilipotolewa na Iceland, lakini mtu huyo kutoka taifa la Croydon anakwenda kufundisha klabu aliyoichezea akiwa kijana mdogo miaka ya 1960.
Kuondoka kwa De Boer pia kutamfanya na Sammy Lee aondoke klabuni hapo, ambaye aliingia kwenye klabu hiyo pamoja na Allardyce, na Ray Lewington anawasili katika benchi la Ufundi la Hodgson.
0 comments:
Post a Comment