Na Mwandishi Wetu, PEMBA
BAO pekee la beki wa kushoto, Mwinyi Hajji Mngwali limeipa ushindi wa 1-0 Yanga SC katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba leo.
Huo unakuwa ushindi wa pili mfululizo na wa 1-0 pia katika kambi ya Yanga kisiwani Pemba kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wa jadi, Simba Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya Alhamisi kuifunga Chipukizi 1-0, bao pekee la Ibrahim Hajib.
Na kwa ujumla huo ni mchezo wa tatu kwa Yanga visiwani Zanzibar, baada ya Jumapili ya wiki iliyopita kuifunga Mlandege mabao 2-0 Uwanja wa Amaan, Zanzibar mabao ya Hajib na Mzimbabwe Donald Ngoma.
Katika mchezo wa leo Gombani, Mngwali alifunga bao hilo pekee dakika ya nne tu ya mchezo huo kwa shuti zuri la mpira wa adhabu kutoka upande wa kushoto wa Uwanja.
Kocha Mzambia, George Lwandamina leo alipanga vikosi viwili tofauti kila kipindi, lakini kile kilichoonekana kusheheni nyota wenye vipaji na uzoefu zaidi ndicho kiliishia kucheza soka ya kuvutia bila kufunga bao kipindi cha pili.
Hajib alikaribia kufunga bao la tatu mfululizo katika mechi tatu za Yanga baada ya kupiga juu ya lango dakika ya 88 kufuatia kazi nzuri ya kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko.
Vikosi vya Yanga SC leo vikulikuwa; kipindi cha kwanza; Ramadhani Kabwili, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Abdallah Hajji ‘Ninja’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’/Pato Ngonyani dk34, Maka Edward, Pius Buswita, Said Juma ‘Makapu’, Amissi Tambwe/Said Mussa dk34, Matheo Anthony na Juma Mahadhi/Yussuf Mhilu dk34.
Kipindi cha pili; Youthe Rostand, Hassan Kessy/Juma Abdul dk70, Gardiel Michael, Kevin Yondan, Andrew Vincent ‘Dante’, Papy Kabamba Tshisbimbi, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Ibrahim Hajib, Emmanuel Martin na Raphael Daudi.

0 comments:
Post a Comment