Mkongwe Robin van Persie amerejeshwa kikosini Uholanzi kwa ajili ya michezo ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa na Bulgaria PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KOCHA wa Uholanzi, Dick Advocaat amemrejesha kikosini mshambuliaji mkongwe, Robin van Persie kwa ajili ya michezo migumu wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa na Bulgaria.
Mshambuliaji wa Fenerbahce, Van Persie alicheza mechi yake ya mwisho na ya 101 ya kimataifa Oktoba mwaka 2015.
Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal na Manchester United mwenye umri wa miaka 34 ndiye anayeongoza kwa ufungaji katika timu yake ya taifa, akiwa amefunga mabao 50 na sasa Uholanzi inamhitaji tena kikosini kurejea kuzisaka nyavu.
Baada ya mechi sita, Uholanzi inashika nafasi ya tatu katika Kundi A, ikizidiwa pointi tatu na vinara, Sweden, wanaoongoza kundi hilo kwa wastani wa mabao dhidi ya Ufaransa. Ni mshindi wa kundi pekee anayejihakikishia nafasi ya kwenda Kombe la Dunia la Urusi.
Mchezaji anayetakiwa na Liverpool, Virgil van Dijk, ambaye hajacheza hata mechi moja Southampton msimu huu akilazimisha kuondoka, hajaitwa.
Uholanzi itacheza na Ufaransa Alhamisi mjini Saint-Denis kabla ya kurudi Amsterdam kumenyana na Bulgaria Septemba 3.
0 comments:
Post a Comment