// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TFF YAMSAFISHA CHIRWA NA KUMRUHUSU KUCHEZA LIGI KUU, MSUVA APEWA ONYO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TFF YAMSAFISHA CHIRWA NA KUMRUHUSU KUCHEZA LIGI KUU, MSUVA APEWA ONYO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, August 31, 2017

    TFF YAMSAFISHA CHIRWA NA KUMRUHUSU KUCHEZA LIGI KUU, MSUVA APEWA ONYO

    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemruhusu kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa kuendelea kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kumkuta hana hatia kufuatia tuhuma za kumshambulia refa.
    Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti, Tarimba Abbas jana mjini Dar es Salaam na uamuzi huo unamnufaisha pia kiungo mpya wa Singida United, Deus Kaseke. 
    Kwa pamoja, wakiwa wachezaji wa Yanga, Chirwa, Kaseke na winga mpya wa Difaa Hassan El- Jadida walidaiwa kumsukuma na kumwangusha refa Ludovic Charles katika mechi namba 236 ya Ligi Kuu iliyokutanisha timu hiyo na wenyeji, Mbao FC walioibuka na ushindi wa 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
    Obrey Chirwa (kushoto) akikabidhiwa mpira na refa Kheri Sasii (kulia) baada ya kufunga mabao manne katika ushindi wa 6-1 dhidi ya Kiluvya United kwenye mechi ya Azam Sports Federation Cup msimu uliopita

    Hata hivyo, baada ya kikao cha jana, wote Kaseke na Chirwa wamekutwa hawana hatia, huku Msuva pekee akitiwa hatiani na kupewa onyo kali.
    Baada ya mchezo huo, Kamati ya Saa 72 ya Bodi ya Ligi ilipitia matukio mbalimbali na kufikia uamuzi wa kuwasimamisha wasubiri suala lao kusikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya TFF.
    Wachezaji hao walidaiwa kufanya kitendo hicho katika mechi hiyo dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Mei 20, 2017 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijni Mwanza. Uamuzi wa Kamati ya Saa 72 ulizingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu.
    Lakini refa, Ludovic Charles naye alipewa onyo kali kwa kutoumudu mchezo kwa mujibu wa Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi. 


    Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Peter Hella amesema kwamba wachezaji wote wapo huru kuendelea na Ligi Kuu baada ya onyo hilo, lakini wanapaswa kujirekebisha
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAMSAFISHA CHIRWA NA KUMRUHUSU KUCHEZA LIGI KUU, MSUVA APEWA ONYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top