// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA NA GULIONI FC LEO AMAAN, YANGA NA JAMHURI KESHO PEMBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA NA GULIONI FC LEO AMAAN, YANGA NA JAMHURI KESHO PEMBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, August 19, 2017

    SIMBA NA GULIONI FC LEO AMAAN, YANGA NA JAMHURI KESHO PEMBA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WATANI wa jadi, Simba na Yanga wikiendi hii wanaendelea na mechi za kujipima nguvu kujiandaa na pambano baina yao kuwania Ngao ya Jamii kuashiria ufunguzi rasmi wa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Timu zote zimeweka kambi visiwani Zanzibar, Simba wakiwa Pemba na Yanga wakiwa Unguja kujiandaa na mchezo wa Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Simba SC leo watacheza mechi yao ya pili katika kambi yao ya Unguja, wakimenyana na Gulioni FC Uwanja wa Amaan, wakitoka kulazimishwa sare ya 0-0 na Mlandege juzi.
    Yanga wao nao watacheza mechi ya pili Zanzibar na ya kwanza Pemba wakimenyana na Jamhuri kesho Uwanja wa Gombani, baada ya Jumapili iliyopita kushinda 2-0 dhidi ya Mlandege Uwanja wa Amaan. Mechi zote zitarushwa na Azam TV. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA GULIONI FC LEO AMAAN, YANGA NA JAMHURI KESHO PEMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top