Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya Simba SC kesho itamenyana na wenyeji, Mlandege katika mchezo wa kirafiki kuanzia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Simba ipo visiwani Zanzibar tangu Jumatatu imeweka kambi kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC Jumatano ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na katika kujiandaa na mchezo huo, Wekundu hao wa Msimbazi watapata mchezo wa kujipima na Mlandege ambayo Jumapili ilifungwa 2-0 usiku wa kesho Uwanja w Amaan.
Katika mchezo dhidi ya Yanga, Mlandege iliruhusu mabao yote kipindi cha pili, mshambuliaji mpya, Ibrahim Hajib aliyesajiliwa kutoka Simba, akifunga bao lake la kwanza katika timu hiyo dakika ya 50, kabla ya kumsetia winga machachari, Emmanuel Mrtin kufunga la pili dakika ya 73.
Kwa Simba, kesho itaingia katika mchezo wa tano, baada ya awali kucheza michezo minne ya kujipima nguvu, ikiwemo miwili katika ziara yake ya Afrika Kusini ambako ilifungwa 1-0 na wenyeji Orlando Pirates kabla ya kutoa sare ya 1-1 na Bidvest.
Agosti 8 katika Simba Day, Wekundu wa Msimbazi walishinda 1-0 dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda Uwanja wa Taifa, bao pekee la Mohammed ‘Mo’ Ibrahim akimalizia pasi ya Emmanuel Okwi aliyefunga bao pekee katika ushindi mwingine wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Jumapili Uwanja wa Taifa pia.
TIMU ya Simba SC kesho itamenyana na wenyeji, Mlandege katika mchezo wa kirafiki kuanzia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Simba ipo visiwani Zanzibar tangu Jumatatu imeweka kambi kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC Jumatano ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na katika kujiandaa na mchezo huo, Wekundu hao wa Msimbazi watapata mchezo wa kujipima na Mlandege ambayo Jumapili ilifungwa 2-0 usiku wa kesho Uwanja w Amaan.
Nyota wa Simba, wakiwemo Jonas Mkude (kulia) na Shiza Kichuya (kushoto) wakiwafuatilia wenzao katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar Jumapili |
Kwa Simba, kesho itaingia katika mchezo wa tano, baada ya awali kucheza michezo minne ya kujipima nguvu, ikiwemo miwili katika ziara yake ya Afrika Kusini ambako ilifungwa 1-0 na wenyeji Orlando Pirates kabla ya kutoa sare ya 1-1 na Bidvest.
Agosti 8 katika Simba Day, Wekundu wa Msimbazi walishinda 1-0 dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda Uwanja wa Taifa, bao pekee la Mohammed ‘Mo’ Ibrahim akimalizia pasi ya Emmanuel Okwi aliyefunga bao pekee katika ushindi mwingine wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Jumapili Uwanja wa Taifa pia.
0 comments:
Post a Comment