// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SAMATTA ATOKEA BENCHI BADO DAKIKA SABA GENK YASHINDA 1-0 NYUMBANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SAMATTA ATOKEA BENCHI BADO DAKIKA SABA GENK YASHINDA 1-0 NYUMBANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, August 27, 2017

    SAMATTA ATOKEA BENCHI BADO DAKIKA SABA GENK YASHINDA 1-0 NYUMBANI

    Na Mwandishi Wetu, GENK
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana aalicheza kwa dakika saba baada ya kutokea benchi, timu yake, KRC Genk ikishinda 1-0 nyumbani dhidi ya Mechelen katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A, Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena, Genk.
    Samatta aliingia dakika ya 83 kuchukua nafasi ya mshambuliaji kinda wa miaka 21, Mdenmark, Marcus Ingvartsen katika mchezo ambao bao pekee la ushindi la Genk lilifungwa na kiungo kutoka Hispania, Alejandro Pozuelo Melero dakika ya 38.
    Huo unakuwa mchezo wa 60 kwa Samatta katika mashindano tangu Januari mwaka jana alipojiunga na Genk, kati ya hiyo mechi 35 alianza na mechi 22 ametokea benchi.
    Katika mechi hizo, mshambuliaji huyo wa zamani wa African Lyon, zamani Mbagala Market na Simba zote za Dar e Salaam, amefunga jumla ya mabao 21.
    Kikosi cha KRC Genk jana kilikuwa: Vukovic, Uronen, Colley, Brabec, Mata, Berge, Malinovskyi/Heynen dk86, Pozuelo/Aidoo dk91, Writers, Buffalo na Ingvartsen/Samatta dk83.
    KV Mechelen: Coosemans, Vitas, Matthys, Croizet, Zipper, Cocalic/The White dk78, Schoofs, Cobbaut, Filipovic/Kawaya dk68, Rherras/Claes dk68 na Drazic.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA ATOKEA BENCHI BADO DAKIKA SABA GENK YASHINDA 1-0 NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top