Na Mwandishi Wetu, DEURNE
NYOTA ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta imeendelea kung’ara nchini Ubelgiji, baada ya leo kufunga mabao mabao mawili na kuseti mawili, timu yake, KRC Genk ikishinda 5-3 dhidi ya wenyeji, Royal Antwerp FC katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A nchini humo, Uwanja wa Bosuilstadion, Deurne.
Samatta alifunga bao la kwanza dakika nane na la nne dakika ya 41 na akaseti la pili lililofungwa na mshambuliaji Mbelgiji, Leandro Trossard dakika ya 16 na tano ambalo beki Mbelgiji, Dino Arslanagic alijifunga dakika ya 59 wakati bao la tatu la Genk limefungwa na mshambuliaji Mbelgiji, Siebe Schrijvers dakika ya 21.
Mbwana Samatta (katikati) akipongezwa na wenzake leo baada ya kazi nzuri
Mbwana Samatta akipiga kichwa mbele ya beki wa Royal Antwep leo
Mabao ya Antwerp yamefungwa na kiungo Mbelgiji, Joeri Dequevy dakika ya 24, mshambuliaji Mghana, William Owusu Acheampong dakika ya 79 na Arslanagic dakika ya 81.
Huo unakuwa mchezo wa 58 kwa Samatta katika mashindano tangu Januari mwaka jana alipojiunga na Genk, kati ya hiyo mechi 34 alianza na mechi 21 alitokea benchi.
Katika mechi hizo, mshambuliaji huyo wa zamani wa African Lyon, zamani Mbagala Market na Simba zote za Dar e Salaam, amefunga jumla ya mabao 21.
Kikosi cha Royal Antwerp FC kilikuwa: Bolat, Kone/Randriambololona dk57, Jaadi, Dequevy/Limbombe dk84, Arslanagic, Hairemans, Batubinsika, Duplus, Corryn, Haroun, Oulare/Owusu dk62.
KRC Genk; Vukovic, Maehle, Brabec, Colley, Khammas, Malinovskyi/Heynen

0 comments:
Post a Comment