MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amefungiea mechi tano na kupigwa faini ya Pauni 2,700 kwa kumsukuma refa, Ricardo de Burgos Bergoetxea baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
Ronaldo alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 82 baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano jana katika mchezo wa kwanza wa Super Cup ya Hispania Uwanja wa Camp Nou, Real Madrid ikishinda 3-1 dhidi ya wenyeji, Barcelona.
Mreno huyo alionyeshwa kadi ya kwanza ya njano dakika moja iliyotangulia baada ya kuvua jezi wakati wa kushangilia bao la pili la timu yake alilofunga dakika ya 80 kabla ya kuonyeshwa kadi ya pili kwa kujiangusha kufuatia kukutana na Samuel Umtiti.
Kifungu cha 96 cha kanuni kinasema kwamba mchezaji anayemvaa refa kwa kumvuta, kumsukuma au kumtikisa atahesabika amefanya kosa la kumfanyia vurugu mwamuzi na adhabu yake ni kufungiwa kati ya mechi nne hadi 12.

0 comments:
Post a Comment