Na Canisius Kagabo, KIGALI
KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda, Yannick Mukunzi ameamua kuachana na timu ya Jeshi la Rwanda (APR) na kwenda uraiania kujiunga na Rayon Sports.
Mukunzi amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu ya Azam Rwanda ambao pia, kama mahasimu wao wa jadi, APR ni mabingwa wa zamani wa Kombe la Kagame la Afrika Mashariki na Kati.
Baada ya kumaliza mkataba wake APR FC, Mukunzi hakuweza kufikia makubaliano na timu hiyo juu ya mkataba mopya na kuamua kwenda timu pendwa zaidi Rwanda, Rayon.
Yannick Mukunzi akiwa na jezi ya timu yake mpya, Rayon Sport baada ya kuachana na APR
Yannick Mukunzi ni mchezaji mzoefu na tegemeo la timu ya taifa ya Rwanda, maarufu kama Amavubi, ni kipaji kilichoibuliwa kwenye akademi ya APR FC kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2013.
Na kuondoka kwake APR kwenda Rayon Sports kumewanung’unisha mashabiki wa timu hiyo ambao wameushutumu uongozi umefanya kosa kumuacha fundi huyo wa mpira aende kwa wapinzani.

0 comments:
Post a Comment