TIMU ya Barcelona imepata pigo lingine baada ya mshambuliaji wake tegemeo, Luis Suarez kuumia katika mchezo wa marudiano wa Super Cup ya Hispani jana dhidi ya Real Madrid.
Nyota huyo wa Uruguay alicheza mechi zote Barca ikifungwa jumla ya mabao 5-1 na Real, kwanza 3-1 Camp Nou wiki iliyopita na jana 2-0.
Ni katika mchezo wa jana Uwanja wa Santiago Bernabeu ndipo Suarez alishindwa kumaliza na kulazimika kutoka nje baada ya kuumia kushuhudia mchezo huo akiwa benchi.
"Luis Suarez amepata matatizo kwenye goti la mguu wake wa kulia. Vipimo zaidi atafanyiwa Alhamisi," imesema taarifa ya Barca mapema leo.
Mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez aliumia goti jana katika mchezo wa Super Cup ya Hispania jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez aliumia goti jana katika mchezo wa Super Cup ya Hispania jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Barcelona imempoteza mshambuliaji wake tegemeo, Neymar mwezi huu aliyegamia Paris Saint-Germain ya Ufaranda kwa dau la rekodi, Pauni Milioni 198 na kumuachia wakati mgumu kocha mpya, Ernesto Valverde kuelekea msimu mpya wa La Liga.
Kwa sasa Barcelona inawawania nyota Philippe Coutinho wa Liverpool na Ousmane Dembele wa Borussia Dortmund ili kuiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji na jana usiku Meneja Mkuu wa Barcelona, Pep Segura alisema dili hizo zinakaribia kukamilika.
0 comments:
Post a Comment