Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
RAIS wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi, maarufu kama Mzee Ruksa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio na matembezi ya Rotary Dar Marathon yatakayo fanyika siku ya kumbukumbu ya kifo cha Rais wa awamu ya kwanza, baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Oktoba 14, mwaka huu.
Akizungumza kweye uzinduzi wa mbio hizo leo mjini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa maandalizi ya Rotary kwa kushirikiana na Bank M, Catherinerose Barretto amesema kwamba lengo la mbio na matembezi hayo ni kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika hospital ya CCBRT, ambayo huhudumia matatizo mbalimbali ya ulemavu ili kuiwezesha hosptali hiyo kutoa huduma kwa watu wengi zaidi.
Rais mstaafu wa awamu ya pil, Alhaj Ally Hassan Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio na matembezi ya Rotary Dar Marathon Oktoba 14
Mkurugenzi wa Bank M, Jacqueline Woiso (wa pili kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Rotary Dar Marathon (kulia kwake) wakisaini mkataba wa kushirikiana katika mbio na matembezi hayo
“Tunayo furaha kubwa kuzindua na kusaini mkataba wa kushirikiana na Bank M kama mdhamini mkuu wa matembezi ya mwaka huu na kuna mambo mapya yameongezeka katika ushiriki wa matembezi ya mwaka huu, kwa mara ya kwanza tutakuwa na Marathoni iliyokamilika ya kilomita 42.2.
“Pia tutaongeza urefu wa mzunguko kwa waendesha baiskeli kotoka kilomita 21 hadi kilomita 42.2 na lengo kubwa la mbio na matembezi hayo ni kuchangisha fedha za ujenzi wa kituo cha afya cha CCBRT,” amesema Barrett.
Naye Mkurugenzi wa Bank M, Jacqueline Woiso amesema kwamba wataendelea kutoa ushirikiano kwa Rotary Marathon kwa sababu wamekuwa wakishirikiana katika shuguli mbalimbali za kijamii na maendeleo kwa ujumla.
Katika ushiriki wa mbio na matembezi hayo, watu wakubwa watalipia Sh. 35,000 na watoto Sh. 10,000 na utaratibu wa kununua fomu hizo utatangazwa kwenye vituo mbalimbali.

0 comments:
Post a Comment