// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MSUVA: NAWAAMINI YANGA, NAWAOMBEA KWA MUNGU WASHINDE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MSUVA: NAWAAMINI YANGA, NAWAOMBEA KWA MUNGU WASHINDE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, August 22, 2017

    MSUVA: NAWAAMINI YANGA, NAWAOMBEA KWA MUNGU WASHINDE

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    WINGA wa klabu ya Difaa Hassan El – Jadida amesema anaiamini timu yake ya zamani, Yanga SC inaweza kuibuka na ushindi dhidi ya Simba kesho na anaiombea kwa Mungu ishinde.
    Yanga SC itamenyana na Simba SC kesho jioni kuanzia Saa 11:00 katika mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Bara msimu wa 2017-2018.
    Msuva amekuwa mchezaji wa Yanga SC tangu mwaka 2012 alipotua Jangwani akitokea Moro United kabla ya kuuzwa Difaa Hassan El - Jadida mapema mwezi huu.
    Simon Msuva amedumu Yanga SC tangu mwaka 2012 kabla ya kuuzwa Morocco mapema mwezi huu

    Akiwa na kumbukumbu ya mechi za mahasimu, Msuva ameitakia kila la heri timu yake hiyo ya zamani alipozungumza na Bin Zubeiry Sports – Online kwa simu leo.
    “Ninawaamini, na ninawaombea kwa Mungu washinde,”amesema mchezaji huyo wa kimataifa wa Tanzania leo kutoka nchini Morocco.
    Yanga imerejea Dar es Salaam leo kutoka kisiwani Pemba ilipokuwa imeweka kambi tangu Jumatatu wiki iliyopita ikitokea Zanzibar ilipolala Jumapili baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege, ikishinda 2-0 Uwanja wa Amaan.
    Na Yanga iliwasili Zanzibar Jumapili ikitokea Dar es Salaam ambako ilicheza mechi mbili za kujipima nguvu, ikishinda 3-2 dhidi ya Singida United Uwanja wa Taifa na kufungwa 1-0 na Ruvu Shooting Uwanja wa Azam Complex, baada ya kambi ya wiki mbili mjini Morogoro.  
    Katika kambi yake hiyo ya siku nane kisiwani Pemba, Yanga ilipata mechi mbili nyingine za kujipima nguvu, zote ikishinda 1-0 dhidi ya Chipukizi na Jamhuri Uwanja wa Gombani na sasa inarejea Dar es Salaam kujaribu kushinda taji la kwanza la msimu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSUVA: NAWAAMINI YANGA, NAWAOMBEA KWA MUNGU WASHINDE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top