REFA wa Marekani, Robert Byrd ndiye atachezesha pambano la ngumi za kulipwa baina ya Floyd Mayweather na Conor McGregor Agosti 26, mwaka huu.
Na pia imethibitishwa na Tume ya Michezo ya Jimbo la Nevada kwamba wapiganaji hao watatumia glavu za ukubwa oz nane (8oz) katika pambano lao la uzito wa Super Welter lisilo la ubingwa.
Kwa kawaida glavu za ukubwa wa oz 10 ndizo hutumika kwenye mapambano ya mabondia wakubwa ngumi za kulipwa hususan uzito kama huu wa Super Welter.
Byrd ndiye aliyechezesha pambano George Groves akipigwa na Badou Jack mwaka 2015, pamoja na mapambano makubwa katika ushindi wa kwanza wa Andre Ward dhidi ya Sergey Kovalev na ushindi wa Saul Alvarez dhidi ya Miguel Cotto.
Floyd 'Money' Mayweather atapambana na Conor McGregor kwenye ukumbi wa T-Mobile Arena Agosti 26, mwaka huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Refa mwenye heshima kubwa, Kenny Bayless aliyechezesha mapambano matatu yaliyopita ya Mayweather, lakini amepingwa kuchezesha pambano hilo.
McGregor mwenye umri wa miaka 29 ameomba majaji wa kimataifa watumike kwenye pambano hilo la kwanza kwake kwenye ngumi za kulipwa akitokea kwenye mapigano ya kutumia ngumi na meteke ya UFC, tena akipigana ana bondia mwenye uzoefu wa miaka 11 na amempendekeza Mtaliano Guido Cavalleri.
Burt Clements na Dave Moretti, wote wanatoka Marekani, ni miongoni mwa majaji watakaokuwa kazini ukumbi wa T-Mobile Arena mjini Las Vegas, Marekaani siku hiyo.
0 comments:
Post a Comment