MSHAMBULIAJI Alexis Sanchez ataukosa mwanzo wa msimu wa Ligi Kuu ya England kutokana na maumivu ya tumbo.
Akiwa amechelewa kujiunga na wenzake kwa maandalizi ya msimu mpya kutokana na kuwa na timu yake ya taifa, Chile kwenye michuano ya Kombe la FIFA la Mabara, Sanchez hataweza kucheza mechi dhidi ya Leicester City Ijumaa.
Lakini Arsene Wenger amesema mchezaji wake huyo nyota yuko nje kutokana na maumivu. "Ana maumivu madogo tumboni aliyoyapata kwenye mazoezi ya Jumapili asubuhi kabla hajaja Wembley,".
Alexis Sanchez ameumia tumbo na atakosekana kwenye mechi za mwanzoni za msimu mpya wa Ligi Kuu ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA
"Alifanyiwa vipimo siku mbili zilizopita na atakuwa nje kwa muda fulani - sifahamu; wiki mbili au wiki moja zaidi? Lakini hatakuwepo. Nafikiri hatacheza Stoke. Kwetu, Alexis Sanchez ni pigo" alisema Wenger.
Alipoulizwa kama Sanchez, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake atasaini mkataba mpya, Wenger alisema: "Wakati wote inawezekana. Mchezaji anapokuwa katika mwaka wa mwisho (wa mkataba wake) wakati wote tutajaribu kumuongezea," alisema. "Hakuna sababu ya kutofanya hivyo. hatujafika huko bado,"alisema.
0 comments:
Post a Comment