TIMU ya Liverpool imeondoka leo na kikosi cha wachezaji 22 kwenda Ujerumani bila Philippe Coutinho na Daniel Sturridge kwa ajili ya mchezo fwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Hoffenheim.
Kocha Mjerumani, Jurgen Klopp na Jordan Henderson walikiogoza kikosi hicho Uwanja wa Ndege wa Liverpool leo wakati wanajiandaa kuondoka kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya mchujo kesho Kusini Magharibi mwa Ujerumani kabla ya timu hizo kurudiana Jijini Anfield Jumatano ijayo.
Coutinho aliukosa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England wa Liverpool ikitoa sare ya 3-3- na wenyeji, Watford kutokana na maumivu ya mgongo, lakini awali ikachukuliwa kama analazimisha uhamisho wa kwenda Barcelona.
0 comments:
Post a Comment