BONDIA Wladimir Klitschko ameamua kustaafu ngumi na kuzima kabisa uwezekano wa pambano la marudiano na Anthony Joshua.
Mbabe huyo wa Ukraine alishindwa na Joshua wa Uingereza katika pambano la uzito wa juu mwezi Aprili na ilitarajiwa wawili hao wangerudiana mjini Las Vegas, Marekani Novemba 11, mwaka huu.
Lakini akkiwa ana umri wa miaka 41 amemaua kusitisha maisha yake ya ulingoni baada ya miaka 21, akizima mazungumzo yoyote ya pambano na Joshua.
Joshua sasa lazima apigane na mshindani namba moja wa IBF, Kubrat Pulev katika pambano lake lijalo kufuatia tangazo hili.
Wladimir Klitschko ameamua kustaafu ngumi na kuzima kabisa uwezekano wa pambano la marudiano na Anthony Joshua PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Gwiji huyo wa ndondi za uzito wa juu anatungika glavu zake akiwa ana rekodi ya 64-5-0, yaani kupigana mapambano 64 jumla na kupoteza matano na tangu miaka ya 2000 ameshikilia mataji ya IBF, WBA, WBO na IBO.
Umaarufu wa Klitschko ulikuja mwaka 1996 baada ya kushinda Medali ya Dhahabu ya ndondi uzito wa juu kwenye Michezo ya Olimpiki, kabla ya mwaka mmoja baadaye kwenda kupigana pambano lake la kwanza la ngumi za kulipwa akimbwaga kwa Knockout (KO,) Marcus McIntyre.
0 comments:
Post a Comment