TIMU ya Everton imekamilisha usajili wa kiungo Gylfi Sigurdsson kutoka Swansea kwa dau la rekodi, Pauni Milioni 45 baada ya kukamilisha vipimo vyake vya afya jana.
Nyota huyo wa kimataifa wa Iceland amesaini mkataba wa miaka mitano jana Goodison Park ambao atakuwa analipwa mdhahara wa Pauni 100,000 kwa wiki.
Timu ya kocha Ronald Koeman italipa ada ya Pauni Milioni 40 na badaye kumalizia Pauni Milioni 2.5.
Kuwasili kwa Sigurdsson Merseyside kunamaanisha timu ya Koeman sasa imetumia jumla ya Pauni Milioni 144dirisha hili la usajili, huku klabu hiyo ikitarajiwa kushindani ubingwa wa Ligi Kuu ya England katika msimu wa pili wa Mholanzi huyo.
Everton imekamilisha usajili wa Gylfi Sigurdsson kwa dau la rekodi la Pauni Milioni 45 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment