NYOTA wa Juventus, Paulo Dybala atakuwa mchezaji mwingine wa kucheza muda mrefu katika klabu hiyo na kuingia kwenye orodha ya magwiji, kufuatia kupewa jezi namba 10 kuelekea msimu ujao.
Mabingwa hao wa Italia wametangaza habari hizo jana kwamba Muargentina huyo atabadilishiwa jezi namba 21 iliyowahi kuvaliwa na wakali kama Zinedine Zidane na Andrea Pirlo.
Jezi namba 10 iliyowahi kuvaliwa na magwiji kama Alessandro Del Piero na Roberto Baggio imekuwa wazi tanfu kiungo Paul Pogba ahamie Manchester United msimu uliopita.
Paulo Dybala amepewa jezi namba 10 iliyoachwa wazi Paul Pogba PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Ni mpango ambao moja kwa moja unamaanisha The Bianconeri's wamekataa kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia Barcelona kufuatia kuondoka kwa Neymar.
Dhahiri mpango wa Juve ni kutengeneza timu ambayo Dybala ataendelea kuwa nyota mkuu kama wanataka kukata kiu ya muda mrefu ya taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hii itakuwa mara ya kwanza kabisa katika historia yake kuvaa jezi namba 10, ambayo imepata umaarufu mkubwa kwa kuvaliwa na watu kama Diego Maradona, Juan Roman Riquelme, Ariel Ortega na Messi.
Mmoja wa waliokuwa wanavaa jezi hiyo, Del Piero ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter kumpongeza Dyabala na chipukizi huyo akajibu ilikuwa 'heshima'.
0 comments:
Post a Comment