Barcelona imethibitisha kumsajili Paulinho kutoka Guangzhou Evergrande ya China kwa dau la Pauni Milioni 36 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KLABU ya Barcelona imethibitisha kumsajili kiungo Paulinho kutoka klabu ya Guangzhou Evergrande yab Ligi Kuu ya China kwa dau la Pauni 36.5.
Mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham atakwendan kufanyiwa vipimo vya afya ili kukamilisha uhamisho wake Alhamisi kabla ya kutambulishwa rasmi Uwanja wa Nou Camp baadaye siku hiyo.
Katika mkataba, klabu hiyo ya Katalunya imweka dau la kumuuza mchezaji huyo Pauni Milioni 109.
Mbrazil huyo ambaye amekuwa akichezea Guangzhou tangu mwaka 2015, amekuwa akitakiwa mno na Barca na sasa inathibitishwa wamempata.
Mchezaji huyo aliyecheza Spurs yenye maskani yake White Hart Lane kwa misimu miwili baada ya kusajiliwa kwa Pauni Milioni 17 kutoka Corinthians ya kwao sasa anarudi Ulaya kwa gia kubwa.
Alicheza jumla ya mechi 67 wakati wake katika misimu hiyo miwili, akifunga mabao 11, lakini ghafla akauzwa kwa Pauni Milioni 10 kwenda China mwaka 2015.
Barca inamsajili Paulinho baada ya kumuuza Mbrazil mwenzake, Neymar kwa dau la rekodi ya dunia, Pauni Milioni 198 kwenda PSG ya Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment