WINGA wa Bolton Wanderers, Sammy Ameobi atakuwa nje kwa wiki sita baada ya kupata maumivu kidogo kwenye goti.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, aliumia goti katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Stoke City na akalazimika kufanyiwa upasuaji.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Newcastle United, Ameobi amejiunga tena na Bolton Julai 14 baada ya kufunga mabao manne tu katika mechi 28 akicheza kwa mkopo msimu uliopita.
Bolton walianza vibaya kampeni yao ya kuwania kurejea Ligi Kuu England baada ya kufungwa 3-2 nyumbanj na Leeds United Uwanja wa Macron mjini Bolton katika mechi ya ufunguzi ya Championship.

0 comments:
Post a Comment