BONDIA Manny Pacquiao amepata mapokezi ya kishujaa aliporejea Ufilipino jana kufuatia kupoteza pambano kimizengwe dhidi ya mwenyeji Jeff Horn - lakini kocha wake wa muda mrefu, Freddie Roach anaamini ni wakati sahihi kwa mbabe huyo kutungika glavu zake.
Horn alifanya moja ya maajabu makubwa katika kumbukumbu za karibuni alipomshinda na kumvua taji la WBO uzito Welter Jumamosi, katika pambano lililopewa jina 'Battle of Brisbane'.
Bingwa huyo wa madaraja nane ya uzito tofauti wa ngumi duniani amerejea nyumbani kwa wanawe leo baada ya kupigiwa saluti askari wa Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo mjini General Santos.
Bondia huyo aliamini ushindi dhidi ya Muaustralia huyo ungemuwezesha kufikiriwa kwa pambano la marudiano na mpinzani wake, Floyd Mayweather.
Lakini Horn akapewa ushindi wa kutatanisha huko Mfilipino huyo akipoteza pambano la saba katika historia yake kati ya mapambano 68 aliyocheza.
Na Roach, ambaye amekuwa akimfundisha Pacquiao tangu alipohamia Marekani mwaka 2001, wakati umefika labda kwa bondia huyo kutungika glavu zake.
Pacquiao alipendekeza mara tu baada ya pambano kwamba atapigania haki yake ya kupewa pambano la marudano. "Tuna kipengele cha pambano la marudiano. Hakuna tatizo,"amesema bondia huyo mwenye umri wa miaka 38.
Pacquiao hakuwa katika ubora wake wakati wa pambano la 'Battle of Brisbane' lakini — kwa mujibu wa takwimu za CompuBox — alirusha ngumi karibu mara mbili ya zilizotupwa na Horn, ambaye alimaliza pambano jicho lake la kushoto likiwa 'nyng'a nyang'a".
Roach ameomba uchunguzi ufanyike juu ya majaji namna walivyotoa pointi, Waleska Roldan akitoa pointi 117-111 kwa Horn na wengine wawili wakitoa pointi 115-113 kwa Horn huku mbabe huyo wa Australia akipuuza madai kwamba hakustahili ushindi.
0 comments:
Post a Comment