Neymar amerejea mazozini baada ya kususa jana kufuatia kugombana na mchezaji mwenzake, Semedo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MSHAMBULIAJI Mbrazil, Neymar amerejea mazoezi kama kawaida baada ya kususa jana kufuatia kugombana na mchezaji mwenzake mjini Miami, Marekani, lakini hadithi za kuondoka Barcelona zinazidi kukua.
Paris Saint-Germain inataka kumpeleka Angel Di Maria Barcelona pamoja na ada ya Pauni Milioni 195 ili kumpata Neymar kwa dau la rekodi la dunia.
Diario AS limeripoti jana kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United, anaweza kutumika kama chambo katika dili hilo.
Klabu hiyo ya Ufaransa inaona hiyo kama njia ya kuepuka kupigwa bei kubwa ya kumnunua Neymar pamoja na kodi zaidi ya Pauni Milioni 62.
Kwa mujibu wa kifungu cha manunuzi katika dili hili, PSG itatakiwa kumlipa Neymar Pauni Milioni 195 na kisha kutoa kiasi kama hicho kwa ajili ya kuvunja mkataba wake.

0 comments:
Post a Comment