Kocha Pep Guardiola (kushoto) akimkabidhi beki Benjamin Mendy jezi ya Manchester City baada ya kukamilisha uhamisho wake PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KLABU ya Manchester City ya England imefikisha jumla ya Pauni Milioni 133 ilizotumia kusajili mabeki wa pembeni, kufuatia kukamilisha uhamisho wa Benjamin Mendy kutoka Monaco ya Ufaransa.
Mfaransa huyo anakuwa beki wa tatu wa pembeni kusajiliwa katika klabu hiyo, baada ya Kyle Walker na Danilo.
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa anajiunga na kikosi cha Pep Guardiola kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 52 baada ya kwenda Los Angeles, Marekani kufanyiwa vipimo vya afya na moja kwa moja kuungana na wachezaji wenzake jana.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 23 amesaini mkataba wa miaka mitano na kukabidhiwa jezi namba 22 atakayokuwa anatumia Uwanja wa Etihad na anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza Jumatano, ambayo itakuwa ya kirafiki dhidi ya Real Madrid mjini LA.
0 comments:
Post a Comment