KLABU ya Chelsea imetangaza kumsajili kipa Muargentina, Willy Caballero kutoka kwa wapinzani, Manchester City.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35, ataimarisha kikosi hicho baada ya kipa wa pili, Asmir Begovic kuhamia Bournemouth.
Kipa huyo wa zamani wa Elche na Malaga amedumu kwa miaka mitatu City, baada ya kuanzia soka yake Boca Juniors ya nyumbani kwao.
Ameiambia tovuti rasmi ya Chelsea kwamba: "Nina furaha sana kujiunga na Chelsea, mabingwa wa England. Naangali mbele namna ya kukutana na jamaa na kuisaidia klabu kupata mafanikio zaidi kwenye msimu unaofuata,".
Ameiambia tovuti rasmi ya Chelsea kwamba: "Nina furaha sana kujiunga na Chelsea, mabingwa wa England. Naangali mbele namna ya kukutana na jamaa na kuisaidia klabu kupata mafanikio zaidi kwenye msimu unaofuata,".
Wakati wake anacheza Manchester, Caballero alishinda fainali ya Kombe la Ligi mwaka 2016 dhidi ya Liverpool baada ya kazi nzuri, ikiwemo kuokoa mikwaju mitatu ya penalti.
Mechi mbili za kukumbukwa msimu uliopita Man City, ni katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa pamoja na kuokoa ya penalti ya mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Falcao kwenye mechi ya kwanza ya hatua ya 16 Bora dhidi ya Monaco.
Nyota huyo aliyewahi kucheza kwa mkopo Arsenal Sarandi, alidaka pia katika kipigo cha City cha 2-1 Stamford Bridge, kwa mara nyingine akionyesha uwezo wake wa kuokoa penalti baada ya kupangua shuti la Eden Hazard, kabla ya Mbelgiji huyo kumalizia mpira uliorudi kuifungia The Bluse bao la ushindi.
0 comments:
Post a Comment