Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga imeamua kuachana na kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima baada ya kutofikia makubaliano naye juu ya mkataba mpya.
Katibu wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba wanaachana na Niyonzima vizuri tu baada ya mazungumzo baina yao kutofikia mwafaka wa mkataba mpya.
“Hata hivyo Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga Sc, lakini hatutaweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia mwafaka katika mazungumzo yetu na yeye licha ya timu yetu kuwa na nia za kuendelea naye kwa misimu miwili ijayo,”amesema.
Aliyekuwa kiongozi wa Yanga, Abdallah Bin Kleb akimkabidhi Haruna Niyonzima jezi ya Yanga wakati anajiunga timu hiyo mwaka 2011 kutoka APR ya Rwanda
Mapema juzi akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online, Niyonzima alisema kwamba yuko kwenye mazungumzo na Yanga juu ya mkataba mpya na wakati huo huo Simba nao wanamuhitaji.
Na tangu jana kumekuwa na taarifa za Haruna kusaini Simba, ingawa yeye mwenyewe kila anapotafuta amekuwa hapatikani kwenye simunyake.
Mzaliwa huyo wa Gisenyi, Rwanda Februari 5, mwaka 1990 alijiunga na Yanga SC mwaka 2011, akitokea APR ya Rwanda aliyoanza kuichezea mwaka 2007 baada ya kujiunga nayo kutoka Rayon Sport iliyomsajili mwaka 2006 kutoka Etincelles iliyomuibua kisoka nchini humo.

0 comments:
Post a Comment