MSHAMBULIAJI Wilfried Bony ni miongoni mwa waliobeba jeneza la mchezaji mwenzake wa zamani wa timu ya taifa ya ya Ivory Coast, Cheick Tiote wakati linawasili jana mchana.
Mwili wa Tiote uliwasili Uwanja wa Ndege wa Port Bouet mjini Abidjan baada ya kusafirishwa kutoka Beijing, ambako alifariki dunia.
Bony alikuwa amevaa fulana yenye picha Tiote ikiwa na maandishi yanayosomeka 'Tembo hawafi' ambayo jina la utani la timu ya taifa ya Ivory Coast.
Kocha wa zamani wa Ivory Coast, Mfaransa Herve Renard pia amehudhuria mazishi hayo sambamba na Rais wa Shirikisho la Soka la Ivory Coast, Augustin Sidy Diallo.
Tiote inasadikiwa alipatwa na mshituko wa moyo Juni 5 wakati wa mazoezi na klabu yake, Beijing Enterprises kabla ya kufariki dunia na awali aliagwa mjini Beijing Jumanne zoezi ambalo lilihudhuriwa na mchezaji mwenzake wa zamani wa Newcastle, Papiss Cisse, ambaye anacheza Shandong Luneng ya China pia.
Tiote alicheza kwa misimu saba Newcastle na anakumbukwa zaidi kwa bao lake la kusawazisha katika sare ya 4-4 na Arsenal Februari mwaka 2011.
Pia amechezea Anderlecht ya Ubelgiji, Twente ya Uholanzi na ameichezea jumla ya mechi 55 timu yake ya tafa, Ivory Coast akiiwezesha pia kushinda na Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment