// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WAGOMBEA 29 TU WAJITOKEZA USAJILI WA UCHAGUZI TFF - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WAGOMBEA 29 TU WAJITOKEZA USAJILI WA UCHAGUZI TFF - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, June 29, 2017

    WAGOMBEA 29 TU WAJITOKEZA USAJILI WA UCHAGUZI TFF

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imefanya usaili kwa wagombea 29 tu kati ya 72 wa nafasi mbalimbali, katika siku ya kwanza ya hatua hiyo muhimu kuelekea uchaguzi mkuu wa shirikisho.
    Wagombea tisa wamechukua fomu za Urais, sita Umakamu wa Rais na 57 Ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda mbalimbali.
    Kabla ya usaili, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Revocatus Kuuli, aliwatangazia wagombea wote kuwa amepokea mapingamzi mawili ambayo ni:-
    Hussein Mwamba ambaye ni Mjumbe kwa sasa wa Kamati ya Utendaji ya TFF, aliyempinga Mussa Sima kuwa amejitokeza kuwania nafasi hiyo katika Kanda ya 10 ya Mikoa ya Dodoma na Singida kuwa hana uzoefu wa miaka mitano.
    Ally Mayay (kulia) amejitokeza kwenye usaili, wakati Geoffrey Nyange 'Kaburu' hakujitokeza
    Wanafamilia wote kwa maana ya Mwamba na Sima walikuwako. Wakaitwa kikaoni, lakini mweka pingamizi - Mwamba aliamua kulitoa pingamizi lake.
    Pingamizi jingine ambalo liliwekwa leo ni kwa Mgombea nafasi ya urais John Kijumbe ambaye anapinga Wallace Karia - Makamu Rais kwa sasa wa TFF kwamba hana sifa za kuwania urais wa TFF kama alivyoomba.
    Hata hivyo, pingamizi hilo halijasikilizwa kwa sababu ya wahusika wote kutokuwako na baada ya kamati kufanya nao mawasiliano, wametangaza kusikiliza pingamizi hilo Jumamosi ambayo ni siku ya mwisho ya usaili.
    Wagombea ambao wamesailiwa leo hadi jioni ya leo Alhamisi kwa upande wa wagombea urais ni Imani Madega na Ally Mayay wakati Wagombea Makamu urais waliosailiwa ni Mtemi Ramadhani na Mulamu Nghambi.
    Kanda Na. 1 Mikoa ya Kagera na Geita; Solum Chama, Kaliro Samson na Leopold 'Taso' Mukebezi, Kanda Na. 2 Mikoa ya Mara na Mwanza; Aaron Nyanda na Samuel Daniel, bado Vedastus Lufano na Ephraim Majinge.
    Kanda Na. 3 Mikoa ya Shinyanga na Simiyu; Mbasha Matutu bado Benista Rugora na Stanslaus Nyongo, Kanda Na. 4 Mikoa ya Arusha na Manyara Omari Walii, Sarah Chao na Peter Temu wote bado.
    Kanda Na. 5 Mikoa ya Kigoma na Tabora; John Kadutu Issa Bukuku, Abubakar Zebo na Francis Michael wote bado, Kanda Na. 6 Mikoa ya Katavi na Rukwa; Baraka Mazengo na Kenneth Pesambili bado.
    Kanda Na. 7 Mikoa ya Mbeya, Songwe na Iringa; Elias Mwanjala, Cyprian Kuyava wakati Erick Ambakisye na Abousuphyan Silliah bado, Kanda Na. 8 Mikoa ya Njombe na Ruvuma; James Mhagama, Golden Sanga, Vincent Majili na Yono Kevela wote bado.
    Kanda Na. 9 Lindi na Mtwara; Athuman Kambi, Dunstan Mkundi, Kanda Na. 10 Mikoa ya Dodoma na Singida; Hussein Mwamba, Mohamed Aden, Mussa Sima na George Benedict Komba,wakati Stewart Masima na Ally Suru bado.
    Kanda Na. 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro; Gabriel Mkwawe tayari wakati Charles Mwakambaya, Francis Ndulane na Hassan Othman ‘Hassanol’ bado, Kanda ya 12. Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga;
    Khalid Mohamed tayari wakati Goodluck Moshi na Thabit Kandoro bado.
    Kanda Na. 13 Mkoa wa Dar es Salaam, Emmanuel Ashery, Shaffih Dauda, Mussa Kisoky, Lameck Nyambaya, Jamhuri Kihwelo, Saad Kawemba tayari wakati Bakari Malima, Ayoub Nyenzi, Saleh Alawi, Ramadhani Nassib,  Aziz Khalfan, Abdul Sauko, Peter Mhinzi, Ally Kamtande na Said Tully bado.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAGOMBEA 29 TU WAJITOKEZA USAJILI WA UCHAGUZI TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top