MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Chile Alexis Sanchez na kiungo Mjerumani, Mesut Ozil wameungana kuitia presha Arsenal iwaongezee mishahara hadi Pauni 300,000 kwa wiki mmoja.
Wawili hao wote wanaringa kusaini mikataba mipya na Gunners na viongozi wa timu hiyo wanasubiri tu maamuzi ya nyota hao.
Na wawili hao wamekuwa taarifa kila mmoja suala lake linavyoendelea ikiwemo masuala binafasi ya kwenye mikataba yao hususan ofa wsanazopewa na klabu.
Arsenal hadi sasa imekwishanasa kwenye mtego wa madai ya Sanchez na Ozil baada ya kubainika imekupali kumpa nyota wa Chile mshahara wa Pauni 270,000 kwa wiki.
Alexis Sanchez na Mesut Ozil wameungana kutaka kila mmja apewe mshahara wa Pauni 300,00 kwa wiki PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment