// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SAMATTA ASHINDWA KUISAIDIA GENK, YACHEZEA KICHAPO 3-1 UBELGIJI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SAMATTA ASHINDWA KUISAIDIA GENK, YACHEZEA KICHAPO 3-1 UBELGIJI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, June 01, 2017

    SAMATTA ASHINDWA KUISAIDIA GENK, YACHEZEA KICHAPO 3-1 UBELGIJI

    Na Mwandishi Wetu, OOSTENDE
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana ameshindwa kuisaidia timu yake, KRC Genk ikichapwa mabao 3-1 na wenyeji, KV Oostende katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Versluys Arena mjini Oostende.
    Mabao ya wenyeji jana yamefungwa na mshambuliaji Mnigeria Joseph Akpala dakika ya 27, mkongwe wa Jamhuri ya Czech, David Rozehnal dakika ya 32 na kiungo wa Afrika Kusini, Andile Ernest Jali dakika ya 51, wakati la Genk lilifungwa na kinda Mbelgiji, Siebe Schrijvers mwenye umri wa miaka 20 kwa penalti dakika ya 44.
    Jana Samatta amecheza mechi ya 60 akiwa amefunga mabao 20 tangu amejiunga na Genk Januari mwaka jana akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kati ya hizo mechi 18 alicheza msimu uliopita na 42 msimu huu na kati ya hiyo, ni michezo 38 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 28 msimu huu.
    Mechi 21 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 13 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita msimu huu na katika mabao yake 20, 15 amefunga msimu huu na matano msimu uliopita.
    Kikosicha KV Oostende kilikuwa: Proton, Milic, Tomasevic, Rozehnal, Capon, Siani/Vandendriessche dk45, Jali, Berrier/Canesin dk88, Musona, Marusic na Akpala/Ozkan dk84.
    KRC Genk: Ryan, Uronen, Colley, Brabec, Castagne, Berge, Writers, Malinovskyi/Heynen dk45 Boetius, Buffalo/Naranjo dk72 na Samatta.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA ASHINDWA KUISAIDIA GENK, YACHEZEA KICHAPO 3-1 UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top