KIUNGO wa zamani wa Chelsea, Oscar jana alijikuta akigombewa kama mpira a kona baada ya mechi kati ya timu yake, Shanghai SIPG na Guangzhou R&F iliyoisha kwa sare ya 1-1.
Oscar amekuwa akifurahia maisha tangu amejiunga na Shanghai Januari na mwanasoka huyo wa kimataifa wa Brazil jana aliendeleza na kazi yake China na kujikuta anapambana na wachezaji wawili Uwanja wa Yuexiushan.
Baada ya kumsetia mchezaji mwenzake, Hulk kufunga bao la kusawazisha kipindi cha kwanza, Oscar baadaye akapatwa na jazba na kuwababua na mpira kwa mashuti mawili mfululizo wachezaji wa timu pinzani.
Wachezaji wa Guangzhou nao wakakasirika na kumvaa kuanza kumshambulia Mbrazil huyo kabla ya wahezaji wenzake Oscar wa Shanghai SIPG nao kwenda kumsaidia mwenzao, hivyo kufanya vita ya mapigano ya watu wote 22 waliikuwa uwanjani.
Walitupiana makonde kadhaa huku wachezaji wa Shanghai wakionekana kumsaidia Oscar, ambaye alikuwa bado amelala chini ya kushambuliwa na wapinzani.
Baada ya vurugu hizo kutulizwa na wachezaji hao kuachanishwa, Li Tixiang alitolewa kwa kadi nyekundu sawa na Fu Huan, huku Oscar akinusurika adhabu yoyote.
Baada ya sare hiyo ya 1-1, Shanghai SIPG inabaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya China - ikizidiwa pointi nne na vinara Guangzhou Evergrande.
0 comments:
Post a Comment